Exodus 25:23-30

Meza Ya Mikate Ya Wonyesho

(Kutoka 37:10-16)

23 a“Tengeneza meza ya mbao za mshita yenye urefu wa dhiraa mbili,
Dhiraa mbili ni sawa na sentimita 90.
upana wa dhiraa moja, na kimo cha dhiraa moja na nusu.
24Ifunike kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. 25Kisha tengeneza upapi wenye upana wa nyanda nne,
Nyanda nne ni sawa na sentimita 8.
na ufanyie ule upapi ukingo wa dhahabu kuuzunguka pande zote.
26Tengeneza pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na uzifungie kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne. 27Pete hizo zitakuwa karibu na ukingo ule ili kuishikilia ile mipiko itakayotumika kuibebea hiyo meza. 28Tengeneza mipiko hiyo kwa mbao za mshita, uifunike na dhahabu, uitumie kubeba hiyo meza. 29 dTengeneza sahani zake na masinia yake kwa dhahabu safi, pamoja na bilauri na bakuli zake kwa ajili ya kumiminia sadaka. 30 eUtaweka mikate ya Wonyesho juu ya meza hii iwe mbele yangu daima.

Copyright information for SwhNEN